Kocha Arsenal, Arsene Wenger amesema Michael Carrick ndiye
chaguo lake kati ya wachezaji sita wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa ligi
kuu ya England. Wenger aliyasema hayo alipokuwa akihojiwa na The Sun, baada ya
kuulizwa nani ni mwanasoka bora wa ligi kuu ya England mwaka huu, Wenger
alijibu kwa kusema ‘mimi nampa Carrick, ni mchezaji mzuri, anajua kugawa mipira
na kulinda goli lake kwa umakini, kwa kiwango chake anaweza kucheza na viungo
wa Barcelona bila shida yoyote’. Kabla ya Wenger kuulizwa swali hilo, waandishi wa
habari walifikiria Wenger angemtaja Van Persie kuwa ndiye mchezaji bora lakini
walishangazwa na kauli ya Wenger kumtaja Michael Carrick, lakini kwa kutambua hilo Wenger alielezea sababu zinazomfanya yeye amchague Carrick, ikiwemo umakini wa Carrick kugawa mipira na kulinda goli. Mbali ya RVP na
Carrick pia wapo Suarez, Bale, Hazard na Mata katika kinyang’anyiro hicho cha
mchezaji bora wa ligi kuu ya England ikiwa Bale na RVP ndiyo wanapewa nafasi
kubwa ya kushinda tuzo hiyo mwaka huu.
No comments:
Post a Comment