Kiungo wa Man City Samir Nasri amemwambia kocha wake Roberto
Mancini kuwa kwasasa amerudi kwenye kiwango chake. Nasri alisema hayo alipokuwa
akiongea na SportsVibe “nimeshamwambia Mancini kuwa nipo 'fiti' na hata yeye
amekubaliana na mimi, nilikuwa nasumbuliwa na maumuvi kwa kipindi sasa, lakini
nimerudi kwenye “fomu”. Natamani sana ningekuwa nacheza hivi tokea mwanzo wa
msimu ili niisaidie timu yangu, lakini sikuweza kwasababu nilikuwa majeruhi, ila
nimerudi naamini nitaisaidia City kwa kipindi hiki kilichobakia kwenye michezo
ya ligi na FA cup. Katika mchezo wa jana (Man city na Chelsea) nusu
fainali ya FA cup Nasri alionesha mchezo mzuri akiwa amefanikisha pasi 38 kati
ya 49 na pia alifunga goli la kwanza baada ya kuwapiga chenga mabeki wa
Chelsea.
Nasri akipangua ngome ya Chelsea kabla ya kufunga goli katika mchezo wa nusu fainali kati ya Man City na Chelsea, mchezo uliokwisha kwa Man City kuibuka na ushinda wa goli 2-1 |
No comments:
Post a Comment