Monday, April 15, 2013

Ushangiliaji wa Di Canio ni kiboko

Kocha mpya wa Sunderland Paolo Di Canio akiruka juu kwa furaha baada ya Sunderland kufunga goli la pili dhidi ya Newcastle. Canio atakuwa ni kocha wa kwanza kwa ligi ya Uingeraza kuwa na aina hii ya ushangiliaji kwa kuruka na kuteleza kwenye majani kama wafanyavyo wachezaji. Di Canio alifanya hivyo ikiwa ni ushindi wake kwanza toka aanze kuifundisha Sunderland.  
Di Canio akiwa anateleza juu ya majani wakati anashangilia goli la pili ikiwa ni aina ya ushangiliaji aliyonayo Jose Mourinho lakini ushangiliaji wa Di Canio ni wa nguvu zaidi ya Jose. Katika mchezo huu Sunderland walishinda goli 3-0 dhidi ya Newcastle na ushindi ambao umeifanya Sunderland kujiongezea matumaini ya kubaki ligi kuu  

No comments:

Post a Comment