Sunday, April 21, 2013

Tottenham 3 - 1 Man City

Revival: Clint Dempsey celebrates the first of three Tottenham goals in seven minutes against Man City
Dempsey (Tottenham) akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza kati ya magoli matatu yaliyofungwa dakika 15 za mwisho yaliyoifanya Tottenham kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Man City. Matokeo haya yanaifanya Tottenham irudishe matumaini yake ya kuwania nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi wakiwa kwenye ushindani mkali dhidi Chelsea na Arsenal. Tottenham bado wapo nafasi ya tano wakiwa na pointi 61 wakati Chelsea wanaocheza na Liverpool leo wapo nafasi ya nne na pointi 61 na Arsenal nafasi ya tatu pointi 63. Chelsea itahitajika kushinda mchezo wa leo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kushiriki UEFA msimu ujao.  

No comments:

Post a Comment