Club ya Yanga inatarajia kuwakosa wachezaji wake watano katika mechi ya ligi kuu dhidi ya JKT Oljoro utakaofanyika jumamosi ijayo kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Yanga itawakosa Jerry Tegete, Stephan Mwasyika, Omega Seme na Ladslaus Mbogo ambao ni majeruhi wanaoendelea na matibabu. Yanga pia itamkosa beki wake mahiri Mbuyu Twite anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano. Wakati huo huo, timu ya Yanga leo imeendelea na mazoezi ya nguvu katika viwanja vya Loyola ili kujiaanda na mchezo huo dhidi ya JKT, mchezo ambao Yanga italazimika kushinda ili kujiwekea mazingira mazuri zaidi ya kuchukua ubingwa. Katika mchezo wa raundi ya kwanza Yanga ilishinda kwa goli moja kwa bila dhidi ya JKT, goli lililofungwa na Mbuyu Twite. Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 49 wakati JKT ipo nafasi ya nane na pointi 28.
Wachezaji wa Yanga wakiwa kwenye mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola (Picha kwa hisani ya Yanga) |
No comments:
Post a Comment