Michuano ya mbio za magari Chinese Grand Prix zinatarajiwa
kufanyika wikiendi hii katika jiji la Shanghai nchini China huku vita baridi ya
kimawazo ikiendelea kuwazonga madereva tegemezi wa timu ya Red Bull, Mark
Webber na Sebastian Vettel. Mgogoro wa Webber na Vettel uliibuka katika mbio za
Malaysia wiki tatu zilizopita baada ya Vettel kukiuka amri aliyopewa na
kiongozi ya timu yake asimpite Webber. Lakini katika michuano hiyo Vettel
alimpita Webber akiwa kwenye spidi kali iliyotaka kusababisha ajali. Tokeo siku
hiyo Webber na Vettel hajaweza kuelewana mbali ya Vettel kuomba msamaha mara
kadhaa.
Vettel akimpita Webber kwenye michuano ya Malaysia, kitendo ambacho kimesababisha mgongano baina yao hadi sasa |
Webber na Vettel wakiwa wamechuniana baada ya mbio za Malaysia |
Wikiendi hii Red Bull itawategemea Webber na Vettel katika michuano ya China lakini mgogoro uliopo baina yao unaweza kuleta adhari kwa timu ya Red Bull ikiwemo ajali kwani Webber atataka kulipiza kisasi kwa Vettel mazingira yatakayo sababisha kupoteza pointi muhimu na kuwapa faida wapinzani.
No comments:
Post a Comment