Wednesday, May 22, 2013

Abidal kuondoka Barcelona mwezi Juni

Eric Abidal wa Barcelona anatarajiwa kutangaza kuhama klabu hiyo mwezi ujao baada ya kukubaliana na uongozi wa klabu. Abidal mwenye miaka 33 anatarajiwa kuhamia kwenye klabu moja nchini Ufaransa (jina halijatajwa) baada ya mkataba wake na Barcelona kuisha ili aweze kuwa karibu na familia yake kwa kipindi hiki ambacho bado anatibiwa kansa. Abidal ameshafanyiwa upasuaji mara mbili kutibiwa kansa ya ini jambo ambalo limemfanya arudi kwao nchini Ufaransa ambapo atakuwa karibu zaidi na familia yake. Taarifa rasmi za kuondoka kwa Abidal zitatangazwa mwishoni mwa mwezi Juni na mkurugenzi wa michezo Andoni Zubizarreta. Abidal alijiunga na Barcelona mwaka 2007 akitokea Lyon na hadi sasa ameshacheza mechi 124 , ameshinda makombe ya ligi mara nne, UEFA champions mara mbili na FIFA club cup mara mbili. 

No comments:

Post a Comment