Wednesday, May 22, 2013

Usajili wa Ngassa umeanza kuleta mgongano

Usajili wa Ngassa kwenda Yanga umeanza kuleta mgongano baada ya viongozi wa Simba kusema Ngassa bado ana mkataba na Simba. Maneno hayo yalisemwa na mwenyekiti wa kamati ya usajili Hans Pope akisema “ Ngassa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Simba, na amefanya makosa kusajili Yanga, tutapeleka malalamiko yetu TFF”. Vilevile, mwenyekiti wa klabu hiyo Aden Rage katika kusisitiza jambo hilo amesema “kwasasa tunangojea muda wa usajili ufike ili twende TFF kupeleka hoja yetu, kwasababu mkataba wa Ngassa upo ofisi za TFF, hatutaki kulumbana wakati kila kitu kipo wazi, sisi tunafuata sheria, tuwe wavumilivu hadi muda wa usajili ufike”. Lakini Ngassa mwenyewe alipohojiwa kuhusiana na jambo hili alithibitisha kuwa yeye hana mkataba wowote na klabu ya Simba wala Azam na kusema kwasasa yupo huru ndiyo maana alijiunga na Yanga. Klabu ya Yanga ilitangaza rasmi kumsajili mcheziji huyo rasmi wiki hii akitokea Simba ambapo alikuwa akicheza kwa mkopo na kuamua kusaini mkataba mpya na Yanga baada ya mkataba wake na Azam kuisha. Sakata hili la Ngassa linatarajiwa kuisha muda wa usajili utakapofika ambapo kila kitu kitawekwa wazi na kujua kama kweli Ngassa bado ana mkataba na Simba, na kama itajulikana hivyo basi ili Ngassa awe mchezaji huru wa Yanga, Yanga itabidi ilipe fedha za uhamisho kwa Simba kwa kukubaliana na klabu ya Simba. 

No comments:

Post a Comment