Saturday, May 25, 2013

Arsenal bado hawajakata tamaa kwa Rooney

Klabu ya Arsenal bado haijakata tamaa za kumsajili mshambuliaji wa Man utd Wayne Rooney licha ya vipangamizi inavyokutana navyo. Hadi sasa Arsenal ina vipingamizi viwili, cha kwanza ni uongozi wa Man utd ambao haujawa tayari kumuachia Rooney aondoke kwani wanaamini mchezaji huyo bado ni muhimu kwao, lakini kipingamizi cha pili ni mshahara wa Rooney ambao anapokea paundi 250,000 kwa wiki wakati kwa upande wa Arsenal mchezaji anayelipwa zaidi ni Walcott na Podolski ambao wanalipwa paundi 100,000 kwa wiki, hivyo Arsenal bado wanajifikiria kumsajili Rooney na kumlipa mara mbili au tatu zaidi ya wenzake. Katika kulitatua hili Arsenal wameshakubali kuongea na Rooney ili wamlipe paundi 200,000 kwa wiki na vilevile watampa kiasi kingine cha pesa wakati huu wa usajili ili kumshawishi aweze kujiunga na Arsenal. Mpango huu unaonesha kufanikiwa katika kutatua kipingamizi cha mshahara, ila kipingamizi kikubwa ni uongozi wa United ambao hadi sasa haujawa tayari kuongelea uhamisho wa Rooney licha ya kuwa Rooney mwenyewe yupo tayari kuhama United. Kama Arsenal watafanikiwa na mpango huu basi Rooney ndiye atakakuwa mchezaji anayelipwa zaidi Arsenal na kwenye historia yote ya klabu hiyo.   

No comments:

Post a Comment