Wednesday, May 22, 2013

Benchi la mkimbiza Thomas Vermaelen

Beki wa Arsenal Thomas Vermaelen anatarajiwa kujiunga na Barcelona baada ya kukosa namba ya kudumu ndani ya klabu hiyo. Vermaelen anatarajiwa kuuzwa kwa paundi mil 5 licha ya kuwa alinunuliwa kwa paundi mil 10 miaka minne iliyopita akitokea Ajax. Arsenal imefikia uamuzi huo baada ya kuona ni hasara kuendelea kumlipa mshahara wakati Mertesacker na Koscielny wameweza kumudu safu ya ulinzi vyema. Baada ya kumuuza mchezaji huyu Arsenal inatarajia kumsajili Ashley Williams wa Swansea ili kuipa nguvu zaidi safu ya ulinzi. 

No comments:

Post a Comment