Wednesday, May 15, 2013

Pellegrini alisema ataondoka msimu huu- Malaga

Klabu ya Malaga leo imethibitisha kuwa kocha Manuel Pellegrini alishaomba kuhama mwishoni mwa msimu huu na yupo huru kuondoka. Uongozi wa Malaga umesema hayo baada ya uvumi kuwa kocha huyo yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na klabu ya Man city ili kuchukua nafasi ya Mancini. Katika ripoti yake, klabu ya Malaga imesema Pellegrini yupo huru kuondoka bila ya kulipa pesa zozote hata kama mkataba wake unakwisha baada ya miaka miwili ijayo. Vilevile, taarifa za wiki hii zinasema Man city wameshaongea na Pellegrini na wapo kwenye hatua za mwisho kufikia makubaliano hivyo siku yoyote watamtangaza rasmi kuwa kocha mpya wa klabu hiyo. 

No comments:

Post a Comment