Friday, May 31, 2013

Wachezaji wa kigeni wavamia mazoezi ya Simba

Kundi kubwa la wachezaji kutoka nchi za Afrika ya magharibi na nchi za jirani na Tanzania wamejiunga kwenye mazoezi na klabu ya Simba ili waweze kusajiliwa. Wachezaji hao wanatoka kwenye nchi za Senegal, Nigeria, Msumbiji na Kongo DRC. Wachezaji hao wapo nchini kutafuta timu ya kucheza kwenye ligi kuu msimu ujao hivyo wapo kwenye kambi ya Simba kutafuta bahati yao. Akizungumzia wachezaji hao kocha mkuu wa Simba Abdallah Kibadeni alisema “wachezaji wengi wanaonekana wamechoka kwasababu hawajafanya mazoezi kwa muda mrefu, lakini baada ya muda watarudi kwenye kiwango chao, sio wabaya sana, ila nitapendelea kuwa na wachezaji wa ndani ya nchi kuliko wa nje ya nchi, ila kama tutapata mchezaji mzuri tutamchukua”. Soko la wachezaji wa kigeni limekuwa kubwa nchini jambo ambalo linafanya wachezaji wengi wa nchi za Afrika kuja nchini kutafuta ajira jambo ambalo lisiposimamiwa vizuri litadumaza soka la bongo. TFF inapaswa kuendelea kusimamia vyema sheria zake ikiwemo ile inayozitaka klabu zote za Tanzania kusajili wachezaji wasiozidi watatu kutoka nje ili kulinda vipaji vya ndani ya nchi. 

No comments:

Post a Comment