Friday, May 31, 2013

Luis Suarez athibitisha kuhama Liverpool

Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez leo amethibitisha kuwa yupo njiani kuhama klabu hiyo na kujiunga na Real Madrid. Suarez amethibitisha hilo akiwa nchini Uruguay na timu ya taifa kujiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Ufaransa. Suarez alisema “huu ni wakati mzuri kwangu kubadilisha mazingira baada ya misukosuko mingi niliyokumbana nayo nchini England, ila napenda watu wajue sababu yangu kuhama Liverpool sio pesa, ingekuwa ni pesa ningeshahama siku nyingi sana, ila sababu ya mimi kuhama ni familia yangu pamoja na vyombo vya habari. Vyombo vya habari vimekuwa vikikuza sana matukio yangu kiasi cha kufanya jambo dogo kuwa kubwa, nimeshapatwa na misukosuko mingi sana, sasa nataka kubadilisha mazingira ili niwe huru mimi na familia yangu, ila napenda kutumia muda huu kuwashukuru sana mashabiki wote wa Liverpool na wachezaji wenzangu kwa ujumla kwani nimeishi nao vizuri tokeo nifike, nitawakumbuka daima”. Luis Suarez mbali ya kuelezea sababu ya kuhama Liverpool pia amesema wakala wake tayari ameshaanza mazungumzo na Real Madrid na mambo yakiwa sawa anategemea kuhama kwa uhamisho wa paundi mil 40. Luis alijiunga na Liverpool kwa paundi mil 22.7 akitokea Ajax mwaka 2011 tokea ajiunge na Liverpool ameshahusika kwenye matukio ya kibaguzi mara mbili na mwishoni mwa msimu huu alipewa adhabu kwa kufungiwa mechi kumi, adhabu ambayo bado anaitumikia hadi sasa baada ya kumng’ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic.  

No comments:

Post a Comment