Friday, May 31, 2013

Madrid kutengeneza sanamu ya Ronaldo

Katika kile kilichoelezwa kuwa Cristiano Ronaldo bado ataendelea kuwepo ndani ya klabu ya Real Madrid, klabu hiyo imechukua uamuzi wa kutengeneza sanamu yake na kuiweka kwenye sehemu ya makumbusho ya klabu hiyo akiwa kama mchezaji wa kukumbukwa kwa mchango wake mkubwa ndani ya klabu hiyo. Ronaldo leo alichukuliwa vipimo na wataalamu wa kutengeneza sanamu za watu tayari kwa kutengeneza sanamu inayofanana na mchezaji huyo. Ronaldo alipoulizwa angependa atengenezwe vipi alisema "ningependa nitokee kawaida kama ambavyo ninavyoonekana nikiwa ndani ya kiwanja, nitengenezwe kwa kuzingatia asili yangu isiwe tofauti sana na jinsi nilivyo". Real Madrid imechukua uamuzi huu ili kumfurahisha Ronaldo aweze kuendelea kuipenda na kuitumikia klabu hiyo hadi hapo mkataba wake utapokwisha mwaka 2015. Katika kipindi hiki cha usajili kumesikika tetesi kuwa Ronaldo anaweza kurudi Man utd au kujiunga na Chelsea akimfuata kocha wake Jose Mourinho jambo ambalo lilimfanya rais wa Madrid Perez kutangaza wazi kuwa Ronaldo sio mchezaji wa kuuzwa na atamuongezea mshahara ili aendelee kuwepo Madrid. Zifuatazo ni baadhi ya picha zinazoonesha Ronaldo akichukuliwa vipimo tayari kwa kutengeneza sanamu yake itakayokuwa na uhalisia wa mwili wake.      
Stay still: Real Madrid striker Cristiano Ronaldo gets measured so a wax figure of him can be made
Concentration: Sculptors work with Cristiano Ronaldo so they can create a wax figure of him
Strike a pose: Real Madrid's Cristiano Ronaldo is measured Mean look: Cristiano Ronaldo

No comments:

Post a Comment