Kocha wa klabu ya Simba Patrick Liewig amesema kikosi cha
Yanga kinastahili pongezi baada ya kushinda mchezo wa jana a goli 2-0. Liewig
aliyasema hayo wakati akihojiwa baada ya mchezo na kusema “ Yanga walistahili
ushindi kwenye mchezo wa leo kwasababu kikosi chao kilikuwa bora kwa kipindi kizima
cha ligi kuu tofauti na kikosi changu cha Simba ambacho nimeanza kukijenga upya
miezi miwili tu kabla ya mchezo wa leo” . Hata hivyo Liewig aliwasifia vijana
wake kwa kujitahidi kupambana tokeo mwanzo wa mchezo hadi mwisho na kusema Simba
wanajipanga kwa msimu ujao ili kurekebisha makosa yaliyojitokeza msimu huu. Kwa matokeo ya jana ambapo Simba ilifungwa goli 2-0 na Yanga imeifanya Yanga imalize ligi na pointi 60 tofauti ya pointi 15 dhidi ya Simba yenye pointi 45.
No comments:
Post a Comment