David Beckham jana usiku alitoka kiwanjani huku akilia ikiwa ndiyo mechi yake ya mwisho kucheza baada ya kutangaza kustaafu. Beckham alitolewa kwenye kipindi cha pili dakika ya 82 akibadilishana na Lavezzi. Beckham, baada ya kuona kibao kimeonesha yeye ndiye anatoka, alianza kukumbatiana na wachezaji wenzake huku machozi yakimtoka na kutembea hadi kwenye benchi lakini baada ya mchezo kuisha haikuwa tena kilio , wachezaji wa PSG pamoja na Beckham walianza kusherekea ndani ya uwanja wakimuaga mwenzao.
|
Mtu mzima alishindwa kujizuia, anakumbukia enzi zake za kila faulo goli, sasa ni muda wa kuwaachia kijiti wengine inamuuma sana |
|
Atakumbukwa daima kwa utalaamu wake wa kupiga mipira ya faulo, kona na pasi ndefu. |
|
Beckham alivaa viatu vyenye majina ya watoto wake maalumu kwa ajili ya mechi yake ya mwisho (watoto wake ni Brooklyn, Romeo, Cruz na Harper) |
|
Beckham akimkumbatia kocha huku akitoa machozi baada ya kutolewa dk 82 |
Baada ya mechi kuisha ilikuwa ni sherehe sio vilio tena
|
Beckham akiwa na watoto wake Brooklyn, Romeo na Cruz |
|
Wachezaji wa PSG wakimpongeza Beckham kwa kumrusha juu baada ya mechi, kilio chote kilikata |
|
Beckham akiwa na bendera ya Uingereza kuonesha utaifa baada ya mechi |
|
Alipewa tuzo kama shujaa baada ya kucheza kwa muda mrefu |
|
Victoria mke wa Beckham pia alikuwepo kiwanjani |
No comments:
Post a Comment