Thursday, May 16, 2013

Wenger ameopoa kifaa kipya kutoka Barcelona

F-C-Barcelona-A-UE-Bordeta-de-_54352188321_54115221155_600_244
kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amemsajili Josimar Quintero kutoka kwenye akademi ya Barcelona La Masia ambaye anatarajiwa kujiunga na Arsenal mwishoni mwa msimu huu, Josimar mwenye umri wa miaka 16 ni raia wa Ecuador anacheza nafasi ya kiungo licha ya kuwa anaweza pia kucheza kama mshambuliaji. Arsene Wenger ni kocha pekee ambaye anasifika kwa kutambua vipaji vya wachezaji tokea wadogo hasa kutoka Afrika, Ufaransa na Hispania, hivyo usajili huu wa Josimar unategemewa kuja kuwa na faida kubwa kwa Arsenal miaka ya karibuni ikifananishwa na Cesc Fabregas ambaye pia alichukuliwa kutoka Barcelona akiwa mdogo na kwa pesa kidogo lakini baadaye alikuja kuwa mchezaji mkubwa sana kwa Arsenal na baadaye kuuzwa tena kwa Barcelona kwa pesa nyingi.

No comments:

Post a Comment