Thursday, June 27, 2013

Donetsk imesema Mkhitaryan ataondoka kwa £25m

Henrikh Mkhitaryan
Klabu ya Shakhtar Donetsk  imesema ipo tayari kumuuza mchezaji wake Henrikh Mkhitaryan kwa klabu za Liverpool na Dortmund kama zitakubali kulipa kiasi cha paundi mil 25 na sio chini ya hapo. Shakhtar imetoa uamuzi huo wiki hii kutokana na tabia ya utovu wa nidhamu aliyoianzisha mchezaji huyu ya kutoshiriki kwenye mazoezi ili kushinikiza kuhama. Liverpool ilikuwa kwenye hatua za mwisho kumsajili Henrikh lakini kauli ya Shakhtar imeikatisha tamaa Liverpool kwani bajeti ya yao ilikuwa ni paundi mil 19.5 ambayo ni pungufu na ile ambayo Shakhtar wanahitaji. Hata hivyo, wakala wa Liverpool bado yupo nchini Ukraine kuendeleza mazungumzo na uongozi wa Shakhtar, mazungumzo ambayo yanatarajia kufikia muafaka mapema. 

No comments:

Post a Comment