Thursday, June 20, 2013

John Mikel Obi ametangaza kujiunga na Galatasaray

Moving on: John Mikel Obi says he is going to leave Chelsea after many years
Kiungo wa Chelsea Obi Mikel ametangaza rasmi kuhamia klabu ya Galatasaray ya Uturuki msimu ujao. Obi ameyasema hayo alipokuwa akiongea na chombo cha habari cha nchini Uturuki, Sabah, na kusema 'nimeshacheza Chelsea kwa muda mrefu, kwasasa nataka kubadilisha mazingira, na nilipopata ofa ya kujiunga na Gala niliomba ushauri kwa rafiki yangu Drogba, akaniambia Uturuki na Galatasaray ni sehemu nzuri kuishi na klabu ya Gala ina mafanikio makubwa, hivyo nikaona ni vyema msimu ujao niwe pamoja na Gala. Nimeishi vyema na Chelsea wakiwemo washabiki na wachezaji wenzangu, nawashukuru sana, kwani nimeweza kupata mafanikio mengi ikiwemo kushinda vikombe vikubwa vya Ulaya na Uingereza, ninaondoka lakini nitawakumbuka daima'. John Mikel Obi kwasasa ana miaka 26 alijiunga na Chelsea mwaka 2006 na ameshacheza mechi 182 akiwa na Chelsea. 

No comments:

Post a Comment