Thursday, June 6, 2013

Mabasi ya TFF yakamatwa kulipa madeni

Mabasi mawili ya TFF jana yalishikiliwa kwa muda na kampuni ya udalali ya Flamingo baada ya TFF kushindwa kulipa deni lake la shilingi mil 50 dhidi ya Hotel ya Safina Holding. TFF inadaiwa kiasi hicho cha fedha baada ya kuwaweka waamuzi wa michuano ya kombe la Kagame mwaka 2012 katika hoteli hiyo wakati michuano hiyo ilipofanyika nchini Tanzania. Baada ya kurupushani za za takribani masaa manne ya kutaka kuchukua magari hayo TFF ilikubali kulipa kiasi cha shilingi mil 20 kwa makubaliano kuwa pesa zingine zitalipwa baadaye.

No comments:

Post a Comment