Thursday, June 6, 2013

Bolt kushiriki mbio za Rome baada ya kuwa majeruhi

Bingwa wa olimpiki na mshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 100 kwa wanaume Usain Bolt wa Jamaica, anatarajiwa kurejea tena uwanjani baada ya kuuguza jeraha la mguu. Bolt anatarajiwa kurudi uwanjani siku ya alhamisi katika mashindano ya mbio za IAAF Diamond League mjini Rome Italia. Bolt alipata jeraha hilo la mguu mwezi uliopita na anatarajiwa kupamabana vilivyo na mshindi wa medali ya shaba wa olimpiki Justin Gatlin. Muingereza Phillips Idowu ambaye alikosa kushiriki katika michezo ya olimpiki ya London kutokana na jeraha vile vile anatarajiwa kuarejea tena uwanjani kwa mara nyingine tena katika michuano hiyo ya jijini Rome Italia alhamisi ya leo. Michuano hii itakuwa ni ya kwanza kwa mwaka huu kuwakutanisha wakali hawa katika mbio za mita 100 jambo ambalo linangojewa kwa hamu kubwa na wapenzi wa riadha duniani. 

No comments:

Post a Comment