Saturday, June 8, 2013

Napoli yakataa ofa ya Chelsea kwa Cavani

Prolific: Cavani is one of the most highly rated strikers in EuropeKlabu ya Chelsea bado ipo kwenye harakati za kuhakikisha inamsajili mshambuliaji wa Napoli Edinson Cavan kwa paundi mil 40. Mapema wiki hii Chelsea walipeleka maombi yao kwa Napoli lakini raisi wa Napoli Aurelio de Laurentiis alikataa ofa hiyo na kusema Cavani hawezi kuondoka Napoli chini ya paundi mil 53 jambo ambalo liliifanya klabu ya Chelsea kurudi na kujipanga tena. Habari kutoka ndani ya Chelsea kama zilivyoelezewa na SportsMail zinasema, klabu ya Chelsea inajipanga tena kutoa ofa nyingine ya fedha pamoja na Torres juu ili kumpata Cavani licha ya kuwa klabu ya Napoli inapendelea ofa ya Man city ambayo itajumuisha fedha pamoja na Edin Dzeko. Mbali ya Cavani, klabu ya Chelsea pia ipo kwenye hatua za mwisho za kumsajili mshambuliaji wa Fiorentina Stevan Jovetic kwa paundi mil 25.5, lakini mchezaji huyu usajili wake unasuasua kwani chaguo la kwanza la Mourinho ni Cavani. Mbali ya Cavani na Jovetic, Mourinho pia amewahitaji Dzeko na Hulk kwa ajili ya msimu ujao wa ligi na michuano ya Ulaya. 

No comments:

Post a Comment