Saturday, June 8, 2013

Goli la uzembe la kipa wa Sudan dhidi ya Ghana

Golikipa wa timu ya Taifa ya Sudan, Abdel Rahman Ali Ibrahim jana tarehe 7/6/13 alijikuta anajifunga kizembe baada ya kushindwa kuzuia kona iliyopigwa na Sulley Muntari wa Ghana katika mechi ya nne kwenye michuano ya kuwania kufuzu kombe la dunia nchini Brazil. Kabla ya kipa kujifunga matokeo yalikuwa Ghana inaongoza kwa goli 2-1. Hadi mwisho wa mchezo Ghana 3-1 Sudan, matokeo ambayo yanaifanya Ghana ifikishe pointi 9 ikiwa kileleni, Zambia pointi 7, Lesotho pointi 2 na Sudan inashika mkia kwa pointi 1. 

Angalia goli hilo alilojifunga Abdel

No comments:

Post a Comment