Tuesday, June 4, 2013

Koscielny asema ukweli, amtishia Wenger kuhama

Beki wa klabu ya Arsenal Laurent Koscielny ametangaza wazi dhamira yake ya kuihama klabu hiyo kama uongozi wa Arsenal hautafanya usajili wa kuleta ushindani kwenye ligi na klabu bingwa. Koscielny aliyasema hayo alipokuwa akiongea na Eurosport alipohojiwa kuhusu tetesi zilizopo kuwa anataka kuhama Arsenal “mimi nahitaji kushinda vikombe, nataka niwe na historia za kushinda, naamini safari hii Arsenal wataniwezesha kushinda kwa kufanya usajili wa maana, sitaki kwenda timu yoyote kwasababu Arsenal ni klabu nzuri na inastahili kushinda, Arsenal sio klabu ya kushindania nafasi ya nne, kisaikologia wachezaji tunaadhirika kucheza mechi za kufuzu Uefa champions league kila mara, Arsenal ina uwezo wa kushiriki Uefa champions moja kwa moja na kushinda vikombe, mimi nimeshachoka, safari hii ni ya mwisho kwangu, ikishindikana kushinda vikombe nitakwenda kwingine”. 

Fight on his hands: Arsenal boss Arsene Wenger must do some deals in the transfer market
Fikra hizi za Koscielny sio za kwake pekee bali kuna baadhi ya wachezaji na washabiki wa Arsenal pia wanamawazo kama ya Koscielny, kwani hawafurahishwi na mwenendo wa klabu yao hususani kwenye sera za usajili na malipo kwa wachezaji hali inayosababisha klabu ya Arsenal kukosa ubora wa kishindani dhidi ya klabu zingine za ndani na nje ya Uingereza. Mara ya mwisho klabu ya Arsenal kushinda kombe la ligi ni mwaka 2004 na FA cup mara ya mwisho ni mwaka 2005. Hali ambayo ni tofauti kwa klabu kubwa zingine ambapo Man utd imeshinda ligi msimu huu, Chelsea imeshinda Uefa mwaka jana na Europa msimu huu na Man city ilishinda kombe la ligi mwaka jana. 

No comments:

Post a Comment