Thursday, June 6, 2013

Tanzania imepanda tena kwenye renki za FIFA

Katika takwimu za ubora wa viwango vya soka duniani zilizotolewa na FIFA leo zimeonesha Tanzania imeweza kupanda kwa nafasi saba kutoka nafasi ya 116 hadi nafasi ya 109 duniani na ndani ya Afrika Tanzania imekwea hadi nafasi ya 32 wakati Kenya ikiwa nafasi ya 123 duniani na nafasi ya 35 Afrika na Uganda ipo nafasi ya 93 duniani na nafasi 24 Afrika. Tokea kocha Kim Poulsen aanze kuifundisha Taifa Stars, Tanzania imekuwa ikipanda kwenye renki za FIFA kila mwezi kwani alipoanza kufundisha, Taifa Stars ilikuwa nafasi ya 145 duniani na sasa ipo nafasi ya 109 akiwa ameipandisha kwa nafasi 36 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. Historia inaonesha Tanzania iliwahi kufikia nafasi ya 65 duniani mwaka 1995 ikiwa ndiyo nafasi ya juu iliyowahi kufikia na ilishawahi kushuka hadi nafasi ya 175 mwaka 2005 ikiwa ndiyo nafasi ya chini kuwahi kufikiwa na Tanzania. Hivyo Kim Poulsen ana kazi ya kuivunja rekodi iliyowekwa mwaka 1995 na ataweza kufikia hatua hiyo kama Tanzania itafanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya kufuzu kombe la dunia inayoendelea sasa. Kuangalia orodha nzima ya FIFA bofya hapa

No comments:

Post a Comment