Tuesday, June 18, 2013

Venus ajitoa kwenye Wimbledon mwaka huu

Born winner: Williams has won the competition five times in her career
Bingwa mara tano wa  Wimbledon Venus Williams amejitoa kwenye michuano hiyo mwaka huu kutokana na maumivu ya mgongo aliyonayo. Venus alitoa taarifa hizi kwenye akaunti yake ya Facebook akisema 'kwa bahati mbaya napenda kuwatangazia kuwa sitaweza kushiriki michuano ya Wimbledon mwaka huu, naipenda sana michuano hii na imeniuma kutoshiriki mwaka huu lakini imenibidi kufanya hivi ili niweze kupona mgongo wangu'. Venus ambaye alipatashida kucheza kwenye michuano iliyopita ya French open amefanya uamuzi wa busara kujitoa kwenye Wembledon kwani maumivu yake yalisababisha kutolewa kwenye hatua za mwanzo jambo ambalo linamfanya apoteze heshima yake kwenye tenesi. Wembledon ya mwaka huu inatarajiwa kuanza jumatatu ya wiki ijayo Juni 24 na mdogo wake Venus, Serena Williams ndiye anayetarajiwa kushinda michuano hii. 

No comments:

Post a Comment