Sunday, June 23, 2013

Vita ya Man utd, Arsenal na Rooney kufikia kikomo

Klabu ya Arsenal imejipanga kutuma rasmi maombi ya kumsajili Rooney kwa uongozi wa Man utd licha ya ugumu uliopo wa kumsajili mchezaji huyo. Taarifa kutoka Sportsmail zinasema, Arsenal wamefikia uamuzi huo baada ya tathmini kuonesha kwamba Rooney na Higuain wanaweza kushirikiana vyema kwenye safu ya ushambuliaji, kwa kumchezesha Higuain namba tisa na Rooney namba kumi ili Rooney afanyekazi ya kumlisha na kumuunganisha Higuain na safu ya kiungo. Kutokana na tathimini hii Arsenal wamejipanga kutoa ofa ya paundi mil 20 kama ada ya uhamisho kutoka United, pamoja na kumlipa mshahara wa paundi 220,000 kwa wiki. Mbali na mipango hii ya Arsenal, klabu ya Man utd pia imejipanga kumpatia ofa na mkataba mpya mchezaji huyu wiki ijayo. Kwasasa Rooney ndiye mchezaji mwenye mshahara mkubwa kuliko wachezaji wote nchini England akipokea kitita cha paundi 330,000 kwa wiki, na United wamejipanga kumuongezea zaidi ili kumuondolea vishawishi vya kuhama. Lakini jitihada hizi za United zinaonekana kwenda kinyume na mahitaji ya Rooney kwani anachokihitaji Rooney ni kucheza kwenye safu ya ushambuliaji na wala sio kuongezewa mshahara. Msimu mzima uliokwisha kocha Sir Alex alikuwa kimchezesha Rooney kama kiungo, jambo lililomfanya acheze chini ya kiwango. Hali hii ndiyo inamfanya Rooney kupata ushawishi wa kutaka kuhama United. Msuguano huu kati ya Rooney, Man utd na Arsenal unatarajia kufikia kikomo wiki ijayo baada ya Rooney kuongea na kocha Moyes ili kufikia muafaka, lakini klabu ya Arsenal wanaombea muafaka huo usifikiwe ili mipango ya kumsajili Rooney ifanikiwe.   
Picha inaonesha Sir Alex na msaidizi wake wakimwangalia Rooney aliyekuwa anatoka nje ya kiwanja akiwa na hasira baada ya kufanyiwa mabadiliko kweye mechi kati ya Man utd na West Ham 

No comments:

Post a Comment