Thursday, June 20, 2013

Neymar lazima aongeze uzito - Daktari wa Barcelona

Brilliant: Neymar scored a wonderful left-footed volley, and set up the other goal, in Brazil's 2-0 Confederations Cup win over Mexico
Daktari wa klabu ya Barcelona Ricard Pruna amesema mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Neymar lazima aongeze kilo mbili au zaidi ili aweze kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Barcelona. Pruna ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na BarcaTV kuhusiana na usajili wa Neymar. Pruna alisema "Neymar ana kilo 64.5, kilo hizi lazima aziongeza kwa kilo 2 au zaidi ili kuweza kuwa na stamina ya kutosha kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Barca kwa dakika 90 bila shida yoyote, tumeambiwa Neymar huwa ana kawaida ya kushika uzito wake zaidi ya kilo 64.5, kwasasa hatuwezi kulifanyia kazi jambo hili, ila atakapo rejea kutoka kwenye michuano ya confederation tutalifanyia kazi na atakuwa fiti pindi msimu wa ligi utakapoanza'. Pruna ameyasema hayo, kwani anafahamu tosha kuwa, Neymar atalazimika kupambana na mabeki wenye afya za kutosha ndani ya ligi na kwenye kombe la Ulaya, hivyo ili aweze kupambana nao lazima awe na uzito wa kutosha tofauti na alivyosasa. 

No comments:

Post a Comment