Thursday, June 20, 2013

Watu wajeruhiwa kwenye vurugu kumuona Beckham

David Beckham
Wanafunzi wanne wamejeruhiwa vibaya katika msongamano wa watu walikuwa wanataka kumuona David Beckham aliyefika kwenye chuo cha Shanghai's Tongji nchini China ili kukutana na uongozi wa chuo pamoja na timu ya chuo. Umati huo wa wanafunzi na raia walikuwa wakisukumana ili kumuona na kumgusa Beckham jambo ambalo lilisababisha wengine kuumia vibaya na kupelekwa hospitali. Kufuatia hali hiyo Beckham ilibidi avunje ratiba yake ya kukutana na timu ya chuo hicho kutokana na vurugu zilizokuwepo na kufanya lengo la kwenda chuoni hapo lisifanikiwe. Beckham mwenye kupitia akaunti yake ya Facebook aliwaomba msamaha mashabiki wake wote kwa kushindwa kukutana na kuongea nao kama ilivyopangwa kutokana na hali ya usalama kuwa ndogo. 
Beckham stampede
Moja ya majeruhi akibebwa kupelekwa hospitali 
Policewoman

No comments:

Post a Comment