Wednesday, June 26, 2013

Zidane atangazwa kuwa kocha msaidizi wa Madrid

Klabu ya Real Madrid imemtambulisha rasmi Zinedine Zidane kuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo. Zidane ametangazwa leo wakati kocha mkuu wa klabu hiyo Carlo Ancelotti alipokuwa anatambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari katika tukio lililofanyika kwenye makao makuu ya klabu hiyo Santiago Bernabeu. Kabla ya kuwa kocha msaidizi, Zidane alikuwa ni mshauri wa mambo ya usajili wa klabu hiyo na kazi ambayo anaifanya hadi sasa ni kuhakikisha Gareth Bale wa Tottenham anasajiliwa na Madrid. Baada ya tukio la leo la kukabidhiwa mikoba ya kuifundisha Madrid, Ancelotti na Zidane wataanza rasmi kazi ya kufanya usajili wa wachezaji ikiwemo pia kuongea na Cristiano Ronaldo ambaye anaonekana mguu moja Madrid na mwingine Man utd. 
Big plans: Zidane would love to bring Tottenham star Gareth Bale to Real
Zidane (kushoto) na Ancelotti (kulia) 
Time to shine: Carlo Ancelotti (left) with Madrid president Florentino Perez
Ancelotti akitambulishwa rasmi kwa kukabidhiwa jezi na Raisi wa Madrid Perez (Kulia) 
Helping hand: Zinedine Zidane (left) will be an assistant for Ancelotti at Real Madrid

No comments:

Post a Comment