Jezi ya Real Madrid yenye jina la mchezaji wa Tottenham Gareth Bale imeanza kuuzwa madukani kabla ya mchezaji huyu kujiunga na Madrid. Jezi hii imeonekana kwenye maduka ya Gibraltar, maduka ambayo ni maarufu kwa kuuza vifaa vya michezo. Jambo hili limeichukiza klabu ya Tottenham kwani hakimiliki ya jina la mchezaji huyu bado ipo mikononi mwa Tottenham, hivyo, kuuza jezi ya Madrid yenye jina la Bale ni kuiba hakimiliki ya Tottenham. Hadi sasa usajili wa Bale kwenda Madrid umesisima kwani Tottenham wanahitaji walipwe Euro mil 120, pesa ambazo Madrid wamesema ni nyingi kulinganisha na thamani ya mchezaji mwenyewe.
|
Monday, August 19, 2013
Jezi ya Madrid yenye jina la Bale imeanza kuuzwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment