Saturday, July 27, 2013

Irine azirai baada ya kumaliza mbio London

Mwanariadha wa Kenya wa mbio za masafa marefu Irine Chebet Cheptai amekimbizwa hospitalini baada ya kuzirai katika mbio za London Anniversary Games. Cheptai ambaye alikuwa mmoja wa wanariadha walioshiriki katika mbio za mita elfu tatu alizirai muda mfupi baada ya kumaliza mbio hizo, ambapo alimaliza katika nafasi ya kumi na moja na kwa kutumia dakika nane na sekunde ishirini. Madaktari waliokuwa uwanjani walimtibu mwanariadha huyo aliyekuwa amepoteza fahamu kabla ya kumkimbiza hospitalini kwa matibabu zaidi. Ripoti zinasema Cheptai hatimaye alipata fahamu baada ya kupata matibabu ya hospitalini. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 21 hushiriki katika mbio za mita elfu tano na mwaka huu tayari ameshiriki katika mashindano mawili ya dunia ya IAAF Diamond League. 

Collapsed: Irine Chebet Cheptai was rushed to hospital after collapsing following the 3,000m
Irine akiewa matibabu uwanjani baada ya kuzirai
treatment: Chebet Cheptai left the track unconscious but, according to reports, later regained consciousness in hospital
Irine akiwa kwenye machela kuelekea hospitali
The Kenyan finished 11th in the race
Irine akiwa kwenye mbio kabla ya kuzirai

No comments:

Post a Comment