Wednesday, July 31, 2013

Je utofauti mkubwa wa thamani kati ya Bale na Suarez ni sahihi???

gareth bale v luis suarez premier league 20122013 Golazo! 17 year old Dorin Rotariu (Dinamo Bucharest) v Vaslui
Picha hii inaonesha takwimu za Bale na Suarez kwenye msimu uliopita, ambapo Suarez amemzidi Bale kwenye vipengele vitatu muhimu (kama vinavyoonekana). Takwimu hizi zimetolewa ili kupima thamani na faida ya wachezaji hawa kwa timu zao. Takwimu zinaonesha Suarez amemzidi Bale kwenye kipengele cha magoli, dakika kwa goli na usaidizi, lakini kwa thamani ya sokoni Bale amezidi Suarez, kwani, Tottenham inamuuza Bale kwa paundi mil 100, wakati Liverpool wanahitaji paundi mil 50 kumuuza Suarez. Mjadala mkubwa umeibuka kuhusiana na suala hili, wengi wakisema Suarez alitakiwa kuwa na thamani kubwa kuliko Bale, kwasababu ya vipengele vilivyolipo kwenye takwimu hizi, lakini baadhi ya wachambuzi wa soka wamenasema Bale ana thamani kubwa kuliko Suarez kwasababu ana kasi na uwezo mkubwa wa kubadilisha mchezo kuliko Suarez.  Mdau wangu wa Michezoupdates hata wewe pia utakuwa na maoni yako kuhusu jambo hili, ...Je utofauti mkubwa wa thamani kati ya Bale na Suarez ni sahihi???  au kwavile Real Madrid wanajulikana ni matajiri ndiyo maana Tottenham wanahitaji pesa nyingi?? au Utovu wa nidhamu wa Suarez umechangia kumshusha thamani??? Unaweza kutoa maoni yako kupitia akaunti ya facebook ya michezoupdates.   

No comments:

Post a Comment