Tuesday, July 16, 2013

'Sina mpango wa kusajili mchezaji' - Mourinho

Talking tough: Jose Mourinho looks ahead to his first friendly in his second spell at Chelsea
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kwasasa hana mpango wa kusajili mchezaji yoyote kwani kikosi chake kinajitosheleza. Mourinho ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari nchini Thailand kabla ya mchezo wao dhidi ya Singha XI, Mourinho alisema ‘Tarehe 31 mwezi wa nane ndiyo mwisho wa usajili, muda huo ukifika ukweli utajulikana na hizi tetesi zote zilizopo zitakwisha, ila kwasasa napenda kuwajulisha kuwa, nimeridhika na kikosi nilichonacho, sifikirii kuongeza mchezaji yoyote, wachezaji ninao wafikiria kwasasa ni wachezaji wa Chelsea ambao bado wapo likizo watakao jiunga na sisi tarehe 28. Jukumu langu kubwa la sasa ni kuwajenga wachezaji nilionao ili waweze kucheza kwenye kiwango cha juu na kuwasaidia chipukizi kukuza vipaji vyao. Haya ndiyo malengo yangu ya sasa na sio kusajili mchezaji mwingine. Mourinho aliongea haya ili kuondoa tetesi zilizopo kuwa Chelsea ina mpango wa kumsajili Rooney na wachezaji wengine, jambo ambalo amekanusha. 

No comments:

Post a Comment