Wednesday, July 31, 2013

Picha ya kutengeneza ya Messi yaleta utata

Messi
Gazeti la Pronto la nchini Argentina wiki hii lilitoa habari ilikuwa na picha ya mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi akiwa mrembo mmoja nchini Marekani. Picha hii imesemekana ilipigwa Las Vegas siku ambayo Messi alikuwa kwenye party pamoja na marafiki zake. Habari za tukio hili zimezagaa kwa kasi kubwa nchini Argentina kutokana na sababu kuwa mchezaji huyu hajawahi kuonekana kwenye mazingira ambayo picha hii inaonesha. Sportmail linaripoti kuwa mahusiano ya Messi na mke wake Antonella yalitetereka baada ya Antonella kuiona picha ya mume akiwa na mrembo huyo. Lakini baadaye ikaja kujulikana kuwa picha hii ilikuwa sio ya kweli bali ilitengenezwa kwa kuunganisha picha kama zinavyoonekana kwenye picha za chini. 

Picha zilivyotengenezwa 
 How Lionel Messis pictures with a blonde stripper in Las Vegas were photoshopped
Picha ya kulia imetengenezwa kutoka kwenye picha ya Messi alipokuwa amembeba mtoto wake 
 How Lionel Messis pictures with a blonde stripper in Las Vegas were photoshopped
Picha ya kushoto imetengenezwa kutoka kwenye picha kulia

No comments:

Post a Comment