Wednesday, July 31, 2013

Bale arejea mazoezini baada ya kukaa nje wiki moja

Heading in: Bale pictured leaving his house this morning Heading in: Bale pictured leaving his house this morning
Gareth Bale akitoka nje ya nyumba yake kuelekea kwenye mazoezi baada ya kukaa nje kwa wiki moja na nusu kuugulia majeraha. Wakati Bale anaanza mazoezi, uongozi wa klabu yake bado upo kwenye mazungumzo na klabu ya Real Madrid kuhusu uhamisho wake. Hadi sasa klabu ya Real Madrid imeshatuma maombi ya kumsajili Bale mara tatu lakini yote yamekataliwa. Klabu ya Tottenham imekataa maombi yote ya Madrid ikidai ofa iliyotolewa ni ndogo kuliko dhamani ya Bale na kuitaka Madrid ilipe kiasi cha paundi mil 100, pesa ambazo zimeonekana ni nyingi kwa Madrid. Lakini taarifa zisizo rasmi zinasema Madrid wanatarajia kutoa ofa ya nne ya paundi mil 85 pamoja na wachezaji wawili Di Maria na Fabio ili kukamilisha mahitaji ya Tottenham. Rais wa Madrid Perez pamoja na mwenyekiti wa Tottenham Levy wanatarajia kukutana wiki hii nchini Marekani kwa mazungumzo zaidi. 

Heading in: Gareth Bale returned to Tottenham training on Wednesday morning
Bale akiwa kwenye gari leo asubuhi akielekea kwenye mazoezi 

No comments:

Post a Comment