Andy Murray ameshinda kwa mara ya kwanza Wimbledon akiwa nyumbani baada ya kumpiga kwa seti tatu mfululizo Novak Djokovic 6-4, 7-5, 6-4. Murray anakuwa ni Muingereza wa kwanza kushinda kombe hili baada ya miaka 77 na ataingia kwenye historia ya Waingereza kama mchezaji aliyeweza kufungua ukurasa mpya wa nchi hiyo kwenye ulimwengu wa tenesi tokea mwaka 1936. Murray ambaye ni mchezaji namba mbili duniani kwenye tenesi atakuwa ameongeza pointi zitakazomfanya ashindane na Djokovic ambaye ni namba moja duniani kwa ubora wa tenesi. Wachezaji hawa wanatarajia kupambana tena kwenye Grand Slam iliyobakia mwaka huu US open ambayo itaanza Agosti 26 hadi Septemba 8 mwaka huu. |
Wageni mbalimbali waliohudhuria fainali ya leo
Rooney na mkewe
Cameron - Waziri mkuu England
Victoria mke wa Beckham
No comments:
Post a Comment