Mdhamini mkuu wa klabu za Simba na Yanga, Kampuni ya Kilimanjaro Premium Lager wamekabidhi vifaa vya michezo kwa klabu hizo vitakavyotumika kwa msimu ujao wa ligi unaotarajiwa kuanza mwezi ujao. Vifaa ambavyo klabu hizi zimekabidhiwa ni pamoja na viatu, jezi za mechi na mazoezi, mipira, soksi, gloves na n.k. Wawakilishi wote wa klabu hizi wameipongeza kampuni ya Kilimanjaro kwa kuendelea kuwadhamini na vilevile wamesifia aina ya vifaa vya mwaka huu wakisema vina ubora mzuri kuliko vya msimu uliopita. |
Tuesday, July 9, 2013
Yanga na Simba zakabidhiwa vifaa vya msimu ujao
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment