Monday, August 5, 2013

Man utd yamkosa Ronaldo, aongeza mkataba Madrid

Coy: Cristiano Ronaldo refused to discuss any new deal during his press conference
Mshambuliaji tegemezi wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameongeza mkataba na klabu yake hadi mwaka 2018. Ronaldo na Madrid wamefikia makubaliano haya baada ya mvutano wa muda mrefu, kwani Madrid walikuwa hawapo tayari kuongeza malipo ya CR7. Mkataba huu utamfanya Ronaldo awe mchezaji anayelipwa kuliko wote kwenye ligi ya Hispania akiwa anapokea mshahara wa Euro mil 17 kwa mwaka, pamoja na asilimia 60 za hakimiliki ya picha. Kwa mshahara wa Euro mil 17 kwa mwaka, Cristiano atamzidi Messi kwa Euro mil 1, licha ya kuwa Messi naye anatarajia kuongezwa mshahara ndani ya mwezi huu. Taarifa hizi za kuongeza mkataba hadi mwaka 2018, zinakuwa ni mbaya kwa wadau wa Man utd ambao walitarajia kumuona tena CR7 ndani ya uzi wa United msimu ujao.  
Gazeti namba moja la michezo nchini Hispania, Marca, likiwa limeripoti habari za Ronaldo kuongeza mkataba leo asubuhi. Mbali ya kuongeza mkataba na malipo, CR7 pia amemaliza ugomvi aliokuwa nao na Rais wa Madrid, Perez, baada ya kufanya kikao nchini Marekani kabla ya mechi kati ya Madrid na Everton. 

No comments:

Post a Comment