Thursday, August 1, 2013

Gerrard aongea ukweli kuhusu suala la Suarez

Nahodha wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrard akiongea na Daily Telegraph amethibitisha kuondoka kwa Suarez kutaifanya klabu ya Liverpool kuyumba kwani haitakuwa rahisi kumpata mchezaji mwingine atakayeweza kuziba pengo lake kwenye kipindi kifupi. ' Kuondoka kwa Suarez au kubaki inategemea na yeye mwenyewe, ila kama akiondoka klabu itaathirika kwa kiasi kikubwa kwenye safu ya ushambuliaji, kwasababu Suarez ni mchezaji mzuri mwenye kipaji cha kipekee. Ni vigumu sana kumpata mchezaji kama Suarez katika kipindi kifupi ndiyo maana kama Liverpool tunajitahidi asiondoke. Haijalishi klabu itapata pesa nyingi kiasi gani, kwa maoni yangu naona Suarez asiuzwe, kwasababu, haina maana yoyote kumuuza Suarez kwa klabu ya Arsenal, klabu ambayo ni mpinzani wetu, jambo hili litatufanya tuendelee kuzidiwa mbali na wapinzani wetu kwenye kinyang’anyiro cha ligi. Kuhusu suala la kucheza Champions league ni bora aende Real Madrid au Barcelona, klabu ambazo kwa kawaida zinafanya vizuri kwenye michuano hii, pia nchi ya Hispania ni nzuri kwa watu wa jamii yao kuishi, kwasababu tamaduni za watu wa America ya Kusini na Hispania zinafanana. Hivyo kama hajapata ofa kutoka kwa Madrid au Barcelona, namshauri Suarez abakie Liverpool kwani atafanikiwa zaidi kweye ligi ya Uingereza akiwa na sisi’. Hayo ni maneno ya Gerrard alipokuwa akiongea na Daily Telegraph.

No comments:

Post a Comment