Thursday, August 1, 2013

'Simba tunakubali kuoneshwa live mechi za ligi'

Msemaji wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga leo ameongea na waandishi wa habari ili kuweka wazi msimamo wa klabu ya Simba kuhusu kuoneshwa live kwa mechi za ligi kuu na Azam TV. Bwana Kamwaga alisema ' Sisi kama Simba hatunapingamizi lolote kuoneshwa live mechi za ligi kuu na Azam TV. Klabu ya Simba tunafahamu kuwa kanuni za FIFA na CAF zinaeleza wazi kuwa, vyama vya mpira kwenye nchi husika ndivyo vyenye haki ya kuingia mikataba na vyombo vya habari kuonesha live au kurekodi mechi za ligi. Sijawahi kusikia Man utd wanashirkishwa kuingia mikataba ya kuonesha live mechi zake za Uefa au ligi, dunia nzima hakuna sheria ya kushirikisha vilabu kwenye mikataba, hivyo sisi kama Simba hatuna pingamizi lolote kuoneshwa live mechi zetu'. Wakati klabu ya Simba ikiwa na msimamo huu, klabu ya Yanga kupitia mwenyekiti wake Yusuf Manji wiki hii walitangaza rasmi kupinga kuoneshwa live mechi za ligi kuu na Azam TV kwasababu wao kama Yanga hawakushirikishwa kwenye mchakato wa makubaliano. 

No comments:

Post a Comment