Washambuliaji mahiri wa Tanzania bara Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu tayari wameshajiunga na timu ya taifa Tanzania bara nchini Kenya. Wachezaji hawa wanatarajia kucheza mechi yao ya kwanza kwenye michuano ya Challenge cup dhidi ya Burundi siku ya jumatano tarehe 4 Novemba. Samatta na Ulimwengu hawakuweza kujiunga na Tanzania bara tokea mwanzo wa michuano wakiwa wanaitumikia klabu ya TP Mazembe. Timu ya Tanzania bara inatakiwa kushinda au kutoka sare dhidi ya Burundi ili iweze kusonga mbele kwenye michuano hii. Hadi sasa Tanzania Bara na Zambia ndiyo zinaongoza kundi B zikiwa na pointi 4 wakati Burundi ina point 3 na Somalia hawana pointi.
No comments:
Post a Comment