Nukuu za Jose Mourinho wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu mechi kati ya Chelsea na Man utd.
-"Hatuendi uwanjani kucheza na timu iliyopo nafasi ya kumi na moja kwenye ligi. Tunakwenda kucheza na mabingwa watetezi wa kombe la ligi"
-"Timu ambayo ipo kwenye matatizo (Man utd) ndiyo timu ngumu zaidi kucheza nayo"
-"Kwa jinsi mwenendo wa ligi unavyokwenda nadhani jambo la msingi kwetu ni kujihakikishia nafasi ya nne (top four) kwanza kabla ya kufikiria masuala ya ubingwa"
-"Kuhusu usajili, kikosi chetu kimekamilika sana, nahisi kwa kipindi hiki tutauza zaidi wachezaji kuliko kusajili"
Wachezaji wa Chelsea wakiwa mazoezini kujindaa na mechi dhidi ya Man utd
No comments:
Post a Comment