Tuesday, January 21, 2014

Tetesi za usajili barani Ulaya leo 22 Jan 2014

Heeling effect: Chelsea's Juan Mata is available and he could well spark an upturn in United's fortunes
DailySport linaripoti kuwa klabu ya Chelsea ipo tayari kumuuza kiungo wake Juan Mata kwa Man utd kwa dau la paundi mil 40. Taarifa hizi zimekuja baada ya fununu kutoka ndani ya klabu ya Man utd kuvuja kuwa Moyes kwasasa anamuhitaji Mata ili aweze kuokoa jahazi la Man utd. DailySport limehabarisha kuwa Jose Mourinho amesema yupo tayari kumuuza kiungo wake kama Man utd watakuwa tayari kumnunua kwa paundi mil 40. Taarifa hizi za Mourinho zimeipa nguvu timu ya usajili ya Man utd na wameshaanza maongezi na wakala wa mchezaji huyu ili waweze kufanya usajili mapema iwezekanavyo ikiwa zimebakia siku 10 dirisha dogo kufungwa. Mbali ya Mata ambaye wakati wowote atakuwa mchezaji wa Man utd, klabu ya Man utd pia imeendelea kutajwa kufanya mazungumzo na wachezaji wengine ambao ni Pogba, Vidal na Dante. 

Playing it cool: Bayern Munich defender Dante has confirmed Manchester United are interested in him
Kiungo mkabaji wa Bayern Munich, Dante, amethibitisha kuwa Man utd wanamtaka kwenye dirisha dogo. Mazungumzo bado yanaendelea licha ya kuwa baadhi ya vyombo vya habari vimeshaanza kuripoti kuwa mchezaji huyu tayari amesajiliwa na Man utd. 

DailyMail linasema, kocha wa Arsenal, Arsene Wenger bado anafikiria mbinu za kuweza kumsajili mshambuliaji wa Atl. Madrid, Diego Costa. Mipango ya Arsenal ya kumsajili mchezaji huyu inakuwa migumu kutokana na nafasi ya Atl. Madrid kwenye ligi na Uefa champions. Atl. Madrid ipo kwenye nafasi nzuri kwenye ligi na Uefa champions, sababu ambazo zinaifanya klabu hii kumzuia mchezaji huyu kuondoka. Lakini taarifa zinasema kati ya washambualiji wote Diego Costa ndiye Arsene Wenger amempenda na amewaagiza wasaidizi wake kufanya juu chini waweze kumsajili kwa ada ya paundi mil 30. 


57264 Picture appears on Reddit claiming Mohamed Salah has just rented an apartment in Liverpool for 7 months
The Telegraph linasema klabu ya Liverpool ipo kwenye hatua za mwisho kumsajili Mmisri, Salah anayechezea klabu ya FC Basel Uswis. Taarifa hizi zimekuja baada ya mkataba wa mchezaji huyu wa kupanga nyumba kwa miezi saba kwenye mji wa Liverpool kuvuja. Picha ya mkataba huu imevuja kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo linaashiria kuwa Salah yupo mbioni kujiunga na Liverpool. Klabu ya FC Basel imetajwa kuhitaji kiasi cha paundi mil 12 ili kumuachia Salah kujiunga na Liverpool. 

IU1IiiN Picture appears on Reddit claiming Mohamed Salah has just rented an apartment in Liverpool for 7 months
Mkataba wa Salah wa kukodi nyumba kwenye mji wa Liverpool kwa miezi saba. 

Rosell: Barcelona has nothing to hide over Neymar
Rais wa Barcelona, Sandro Rosell amesema yupo tayari kwenda mahakamani kutoa ushahidi kuhusu fedha kamili zilizotumika kumsajili Neymar. Rosell amesema taarifa zilizotolewa na gazeti la El Mundo kuwa Neymar alisajiliwa kwa Euro mil 95 sio za kweli, ila mchezaji huyo amesajiliwa kwa Euro mil 51 tu. Mkanganyiko wa usajili wa Neymar ulianza chinichini lakini kwasasa umekuwa mkubwa na kufanya washabiki wa klabu hiyo kuanza kuhoji jambo ambalo limeanza kuleta msuguano ndani ya klabu. 

Eden Hazard rules out Chelsea exit
Kiungo wa Chelsea, Eden Hazard ameliambia gazeti la Telefoot kuwa hana mpango wa kuondoka Chelsea kwasasa. Hazard aliongea haya ili kuondoka tetesi zilizopo kuwa anataka kwenda PSG, Hazard alisema 'ninasikia fununu zilizopo mitaani kuwa mimi nataka kujiunga na PSG, taarifa hizo sio za kweli na sina mpango huo. Bado nipo chini ya Mourinho na nina furahia maisha yangu nikiwa na Mourinho hivi sasa'. 

Fernandes: Julio Cesar poised for QPR exit
Golikipa tegemezi wa timu ya taifa ya Brazil, Julio Cesar anategemea kuhama klabu anayoichezea QPR baada ya kusikiliza maoni ya kocha wake wa taifa Scolari. Mapema wiki iliyopita Scolari alisikika akisema 'ili Cesar aweze kupata namba ya kudumu kwenye timu ya taifa lazima apate mechi ngumu za kutosha hivyo ni vyema akahama klabu yake iliyopo ligi daraja la pili nchini England'. Kwa taarifa zilizopo kwenye vyombo vya habari kwasasa, Cesar ametajwa kutaka kurudi Seria A ligi ya Italia licha ya kuwa klabu atakayo kwenda bado haijatajwa. 

No comments:

Post a Comment