Habari za Diego Costa kwenda Chelsea mwishoni mwa msimu huu sasa zimekuwa za uhakika baada ya vyombo vyote vya habari nchini Uingereza na Hispania kuthibitisha jambo hili. Marca walianza kuliongelea, wakafuatia Dailysport lakini kwasasa ni vyombo karibia vyote vimethibitisha. Makubaliano haya ya Chelsea na Atl. Madrid yanamuhusisha pia golikipa wa Chelsea Thibaut Courtois anayechezea Atl. Madrid kwa mkopo, kuwa kuna uwezekano golikipa huyu akajumuishwa kwenye dili la kumsajili Costa. Dailysport limesema, Courtois anaweza kuruhusiwa kujiunga na Atl. Madrid na pesa juu zikaongezwa kumnunua Costa.
Hatimaye Michael Essien asaini mkataba wa kuichezea Ac Milan baada ya dosari za majeraha kutaka kusitisha usajili wake. Klabu ya Ac Milan na Michael Essien zimeweza kufanya makubaliano kwa mchezaji huyo kuichezea Milan ndani ya mkataba wa miezi 18. Usajili huu wa Essien uliingia dosari juzi baada ya madaktari wa Ac Milan kusema Essien ana majeraha kwenye kifundo cha mguu, majeraha ambayo yaliwapa hofu madaktari, lakini kwa kushirikiana na klabu ya Chelsea, mazungumzo yaliweza kufanyika hatimaye Essien kusaini mkataba.
Ndoto za Man utd kumsajili beki wa kushoto wa Everton, Leighton Baines zimekufa baada ya beki huyu kuongeza mkataba wake hadi mwaka 2018. Beki huyu alihitajika kujiunga na Man utd ili kuchukua nafasi ya Evra ambaye ameonekana kiwango chake kimeshuka. Taarifa hizi zitakuwa ni mbaya kwa Moyes ambaye yupo kwenye kipindi cha kujenga kikosi chake kwa kuongeza wachezaji wengi wapya.
Rais mpya wa Barcelona Josep Bartomeu amekiri kuwa klabu yake itamsajili golikipa wa Borussia Monchengladbach, Ter Stegen. Bartomeu aliyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari wikiendi akisema "ni kweli tutamsajili Ter Stegen kwasababu Valdes ataondoka mwishoni wa msimu, hivyo Stegen ndiye tunatarajia ataziba pengo lake. Mbali ya Stegen, kama Barcelona tuna mbadala wa makipa wengine hivyo chaguo letu sio Stegen peke yake ila taarifa zaidi tutaendelea kuzitoa". Barcelona tayari imeshasaini mkataba wa awali na Stegen ili kuchukua mikoba ya Valdes ambaye ni golikipa wa sasa wa Barca anayetarajia kuhama mwishoni mwa msimu huu.
Kocha wa Liverpool Bredan Rodgers ameongea na waandishi wa habari kuhusu usajili wa dirisha dogo. Wiki mbili zilizopita Rodgers alisema hana mpango wa kufanya usajili wowote lakini wiki hii amebadilika baada ya kukabiliwa na majeruhi wengi. Rodgers alisema “ bado tunaangalia nini cha kufanya kwasababu kusajili mchezaji kwenye dirisha dogo ni jambo gumu sasa. Ni kweli kwasasa tunahitaji mchezaji lakini hatuna haraka sana. Tumelazimika kutafuta mchezaji ili kuziba mapengo ya majeruhi, lakini hatuna haraka sana kwasababu sitaki kumsajili mchezaji wa kukaa benchi, nahitamji mchezaji atakayecheza na awe na matokeo mazuri kwenye kikosi changu cha kwanza. Klabu inafanya kila njia ili kupata mchezaji makini kabla ya mwisho wa usajili na nina matumaini kuwa tutafanikiwa kwa hilo". Hayo ni maneno ya Rodgers, na hadi sasa wachezaji waliotajwa kuwindwa na Liverpool ni Adre Gomes, Thomas Ince na Saul Niguez, labda mmoja kati ya hawa anaweza kujiunga na Liverpool.
Jorge Messi (baba mzazi wa Lionel Messi) amesema mtoto wake hana mpango wa kuhama klabu ya Barcelona. Jorge alisema hayo alipokuwa akiongea na gazeti la L'Equipewhen akisema " nimesikia fununu hizo lakini sijui zimetoka wapi. Hakuna kitu kama hicho kuwa Messi atakwenda PSG kwani mkataba wake wa sasa utakwisha 2018. Ni furaha kusikia klabu nyingi ikiwemo PSG kuwa zinamuhitaji Messi lakini kwasasa Messi ni mchezaji wa Barcelona na hatupendi kuwaza tofauti na hilo. Najua mambo ya soka hayatabiriki lakini kila kitu tunamuachia Mungu yeye ndiye mpangaji wa yote". Hayo ni maneno ya Jorge Messi, baba mazazi wa Lionel Messi, kauli yake nahisi itakuwa imetoa jibu zuri kuhusu tetesi zilizokuwepo kuwa Messi anaweza kuhamia PSG.
No comments:
Post a Comment