Sunday, January 19, 2014

Tetesi za usajili wikiendi hii 18-19 Jan 2014

Koke aongeza mkataba wake na Atletico Madrid. Kumbuka mchezaji huyu alikuwa akiwindwa na klabu ya Man utd. Hivyo kuongeza mkataba na Atl. Madrid kunafanya matumaini ya mchezaji huyu kwenda United kufa kabisa. 

 

DailySport linasema kila siku zinavyokwenda mahusiano ya Rooney na uongozi wa Man utd yanazidi kudorora. Rooney ameshapewa mkataba mpya na Man utd lakini hadi sasa bado hajausaini ili kuongeza muda na maslahi yake. Taarifa zinasema tatizo la Rooney ni kuchezeshwa nafasi asiyoipenda kwenye kikosi cha Man utd. Rooney alianza kupagwa kwenye nafasi ya kiungo kwenye msimu wa mwisho wa Sir Alex hadi leo, jambo ambalo linamfanya asiweze kufunga magoli na kumpoteza kwenye ramani ya wafungaji. Jambo hili ndilo linamfanya hadi sasa ajifikirie kuhusu mkataba mpya au kuhama timu. Rooney alishaongelewa kutaka kuhamia Chelsea au Arsenal, lakini uongozi wa Man utd ulikanusha na kusema mchezaji huyu kama atauzwa basi atakwenda klabu ya nje ya England. 

Mata (right) has spent most of the season on the bench
Klabu ya Man utd imejipanga kutoa ofa ya paundi mil 20 ili kumsajili kiungo wa Chelsea, Juan Mata. Mata ambaye anaamini kuwa ni mmoja kati ya viungo bora duniani bado hajaweza kumridhisha kocha wake Jose Mourinho jambo ambalo linamfanya akae benchi kwenye mechi nyingi. Kukaa benchi kwa muda mrefu sambamba na ugomvi alionao dhidi ya Mourinho kumeifanya klabu ya Man utd kushawishika kumsajii mchezaji huyu ndani ya dirisha dogo. Dili hili la Mata limetajwa kumuhusisha pia Rooney ambaye anahitajika na Chelsea. Bado taarifa hazijasema itakuwaje lakini inawezekana Mata na Rooney wakabadilishana na pesa kidogo zikaongezwa. 

 
Alvaro Morata mshambuliaji wa Real Madrid wikiendi hii amesema kuwa hana mpango wa kuondoka ndani ya klabu hiyo. Morata ambaye ametajwa kujiunga na Arsenal au Benfica, ameyasema hayo baada ya mechi kati ya Real Madrid na Real Betis ambapo aliweza kufunga goli la tano. "sina mpango wa kuhama Madrid, nina furaha kuichezea klabu hii". Taarifa hii inakatisha matumaini ya klabu za Arsenal na Benfica ambazo zilionesha nia ya kutaka kumsajili. 


Klabu ya Tottenham ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Lille ili kumsajili winga wa klabu hiyo Kaluo ambaye alijiunga na klabu hiyo hivi karibuni akitokea Chelsea. 


Klabu ya Arsenal inaaendelea kuwasaka wachezaji wa Kijerumani ambapo wiki hii taarifa zinasema klabu hiyo inamuwinda mshambuliaji wa Schalke 04, Julian Draxler. Taarifa kutoka DailyMail zinasema klabu ya Arsenal imetuma ofa ya paundi mil 37 kwa klabu ya Schalke 04 ili kumsajili Draxler. Mbali ya Draxler, klabu ya Arsenal imehusishwa pia na usajili wa Morata na Mirko Vucinic


Mirko Vucinic

No comments:

Post a Comment