Sunday, March 16, 2014

Mbrazil Rivaldo atangaza kustaafu soka


Mkongwe Rivaldo ametangaza kustaafu soka baada ya kucheza kwa kipindi kirefu. Rivaldo ametangaza nia yake ya kustaafu soka wiki hii kupitia akaunti yake ya Instagram akiandika maneno ya majonzi kutokana na mapenzi yake kwenye soka. Rivaldo alisema, ' natokwa na machozi kusema kuwa muda wangu wa kucheza soka umefikia kikomo. Nimepata mafanikio makubwa sana kwa kucheza soka nje na ndani ya Brazil licha ya vikwazo na changamoto nyingi nilizokutana nazo. Mbali ya kushinda vikombe na medali nyingi, pia nimetengeneza historia kwenye mchezo wa soka kitaifa na kimataifa'. Katika maneno yake Rivaldo hakuacha kuitaja klabu ya Barcelona, klabu ambayo ameitaja kama kilelel cha mafanikio yake katika soka. Rivaldo alijiunga na Barcelona akitokea Deportivo La Coruna na kuichezea Barca kwa misimu mitano na kuchinda makombe mawili ya ligi, Copa Del Rey, Uefa Super Cup, mchezaji bora wa ligi ya Hispania na mchezaji bora wa Dunia. Mbali ya Barcelona na Deportivo, Rivaldo pia amezichezea klabu zifuatazo; AC Milan, Cruzeiro, Olympiakos, AEK Athens, Bunyodkor, Sao Paulo, Kabuscorp, Sao Caetano naMogi Mirim. 


No comments:

Post a Comment