Wednesday, March 5, 2014

Ramsey arudi dimbani na mkataba mpya juu

Winner: Arsenal's Aaron Ramsey is due to return to training on Thursday and set to sign a contract extension
Kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey amekubali kusaini mkataba mpya na klabu yake utakaodumu hadi mwaka 2018. Mkataba huu utamuwezesha Ramsey kulipwa paundi 90,000 kwa wiki kutoka paundi 60,000 alizokuwa akilipwa kwenye mkataba wa zamani. Mbali ya kusaini mkataba mpya Ramsey pia anatarajiwa kuanza mazoezi wiki hii na atakuwa fiti kucheza mechi dhidi ya Tottenham kwenye ligi kuu. Ramsey alikuwa majeruhi kwa kipindi kirefu na ameshakosa mechi nyingi muhimu, kurudi kwa mchezaji huyu kipindi hiki ni furaha kwa Arsene Wenger kutokana na umahiri wa mchezaji huyu wa kufunga na kutengeneza magoli. 

No comments:

Post a Comment