Club ya Chelsea ndiyo inaongoza hadi sasa kwa kutenga dau kubwa la kumchukua Yaya kutoka Man City. Imepita wiki mbili sasa toka Yaya Toure na Man City waingie kwenye mzozo wa mkataba. Yaya kupitia wakala wake alisema wanaipa Man City wiki moja kuamua kama watafunga mkataba mpya na Yaya au la. Yaya yupo tayari kuihama Man City kama hawatafikia makubaliano na Man City. Kufuatia hali hii, timu mbalimbali zimekuwa zikimnyemelea Yaya lakini hadi sasa Chelsea ndiyo wanaongoza kwa kutoa dau kubwa zaidi ya wote la dola za kimarekani milioni 22, Chelsea inamuhitaji zaidi Yaya ili kuziba pengo la Frank Lampard anayeweza kuhama mwishoni mwa msimu huu kwenda Galaxy.
No comments:
Post a Comment