Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco (Lions of the Atlas) imeingiza sh. 226,546,000, watazamaji walikuwa 32,614. Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 VAT ni sh. 34,557,864.41, maandalizi ya mchezo sh. 28,450,000, gharama za uchapaji tiketi ni sh. 8,625,641.88, bonasi kwa timu ya Taifa Stars sh. 28,798,220.34, asilimia 15 ya uwanja sh. 18,917,141.01, asilimia 20 ya gharama za mechi sh.25,222,854.67 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 6,305,713.67. Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 71,885,135.82 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,783,428.20 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF. Habari hizi kwa mujibu wa TFF
No comments:
Post a Comment